Tuesday, September 27, 2022

Vidokezo vya Kufanya Likizo Yako Ijayo iwe Rafiki kwa Mazingira

Hatimaye dunia imefunguka na safiri zimeanza tena. Na hilo ni jambo zuri!

Lakini watu kote ulimwenguni wanapotazamia kuondoa uchovu wa miaka miwili, kuna hitaji kubwa zaidi la kuwa mwangalifu zaidi wa mazingira.

Je, huna uhakika jinsi ya kufanya safari zako ziwe salam, endelevu na rafiki kwa mazingira?

Usijali. Tumekuletea masuluhisho na mapendekezo ya usafiri endelevu, bila kujali kama unaelekea fukwe za bahari, mijini au milimani.

Kutembelea Fukwe za Bahari

qvi 1 Ufahamu Wa QNET

Pakia: Ikiwa tayari una nguo za kuogelea, ni vizuri! Lakini ikiwa unahitaji kununua, hakikisha kwamba unapata mavazi yaliyotengenezwa kutoka kwa plastiki iliyosindikwa. Ni endelevu zaidi kuliko nylon ya kawaida. Pia, ingawa kinga ya jua ni muhimu, hakikisha kwamba kinga yako ya jua ni ya kaboni na haina kemikali ambazo ni hatari kwa viumbe vya baharini.

Tofauti na kinga ya jua, ni vizuri kubeba kofia. Haya yatapunguza hitaji la kujipaka kinga ya jua nyingi.

Maandalizi: Si kila fukwe zote zinafanana, na zingine zimekua za kibiashara Zaidi kiasi kwamba wameongeza mkazo wa mazingira. Hata hivyo, kuna idadi kubwa ya maeneo ya bahari yenye maadili, rafiki kwa mazingira na yasiyo na watu wengi sana ambayo unaweza kufikiria kutembelea. Jambo kuu ni kufanya utafiti.

Ukifika hapo: Mchanga na maji ya chumvi kupita kiasi humaanisha mavazi yatahitaji kufuliwa. Lakini unaweza kupunguza uharibifu wa mazingiwa kwa kuchagua kufua kwa mikono na sio machine za kufulia. Pia, kumbuka kuokota takataka na kukaa mbali na matuta ya mchanga! Takataka mara nyingi hupuuzwa na wasafiri. Na pia matuta ya mchanga, ambayo hulinda dhidi ya mmomonyoko wa viumbwe na mazingira ya bahari, ni dhaifu sana na yanaweza kuharibiwa kwa urahisi inapotembea au kuchezewa.

Chagua pakukaa: Haijalishi unaelekea wapi, chagua malazi rafiki kwa mazingira. Prana Resort Nandana huko Koh Samui, ambayo imezindua idadi ya mipango ya uhifadhi katika miaka ya hivi karibuni, ni chaguo bora ikiwa unachagua kutembelea fukwe za Thai. Pia inajivunia spa ya Amezcua.

Kwa safari za mijini

Safari za mijini Ufahamu Wa QNET

Pakia: Kanuni ya 1 ya safari za mjijini ni kupaki kiasi! Ndiyo, mapumziko ya mijini yanaweza kumaanisha kutembelea makumbusho, migahawa na kadhalika. Lakini hauitaji mavazi tofauti kwa kila kitu. Badala yake, paki nguo nyingi ambazo zinaweza kurudiwa na kuendana kwa urahisi. Hakikisha, pia, kwamba una chupa ya maji na mifuko midogo kwenye mizigo yako. Itakufaa unapozunguka.

Maandalizi: Kama ilivyo kwa likizo za ufukweni, inafaa kufikiria kuhusu aina ya likizo unayotaka. Hii itakusaidia kufanya maamuzi muhimu kuhusu mahali pa kwenda na nini cha kufanya ukifika. Kwa bahati nzuri QVI Tripsavr inatoa ofa nzuri mapema. Kwa hivyo kufanya maamuzi mapema kunaweza kukokoa pesa.

Ukifika huko: Unakumbuka vile vibegi vidogo? Naam, sasa ni wakati wa kuzitumia badala ya mifuko ya plastiki. Chupa yako ya maji, wakati huo huo, itahakikisha kuwa una maji kila mara bila kununua maji mara kwa mara. Licha ya hivo, ikiwa utanunua zawadi, jaribu kuzingatia zawadi endelevu iwezekanavyo ili kusaidia biashara za mjini.

Chagua pakukaa: Kuna chaguo nyingi mno inapokuja kwenye safari ya miji mikubwa. Lakini kwa nini usichague jiji kuu la kisasa ambalo pia limejawa na historia na utamaduni, kama vile Antalya, Uturuki? Jiji, ambalo ni mojawapo ya vitovu vya utalii wa mazingira yanayokua kwa kasi Zaidi duniani, ni la kustaajabisha sana, na kuna makao mengi endelevu yanayotolewa. Moja ni Hoteli ya Dogan inayojali jamii na kimazingira, ambayo ipo katikati ya mji wa kihistoria wa Kaleici.

Kwa safari za Nyanda za Juu

Pakia: Hali ya hewa yenye ubaridi zaidi kwenye nyanda za juu hufanya kupaki nguo chache kua zoezi gumu. Lakini hakuna haja ya kuwa na mabegi mengi. Zaidi, fikiria juu ya nguo ambazo una uwezekano wa kuvaa mara nyingi, kisha upakie hizo. Unaweza pia kuvaa nguo zako nzito kwenye ndege. Wakati wa kuzingatia vifaa vya kujitunza kama sabauni za kuoga na kadhalika wakati huo huo, chagua vitu ambavyo ni Rafiki kwa mazingira.

Kujitayarisha: Mamia ya mamilioni ya watalii wanaomiminika katika maeneo ya nyanda za juu kila mwaka wanaweza kusababisha matatizo katika mazingira asilia. Hii haimaanishi kuwa unapaswa kuondoa ratiba za kutembelea haya maeneo. Lakini fikiria kutembelea kipindi ambacho sio cha baridi. Bado utapata furahara ile ile ila ukiwa na watu wachache.

Ukiwa huko: Maeneo mengi ya nyanda za juu yanaweza kufikiwa na magari na mabasi. lakini, ukiwa hapo, jaribu kuzunguka kwa wepesi, tukimaanisha bila usafiri wa gari. Baiskeli na/au pikipiki za umeme kwa kawaida zinapatikana kwa kukodishwa. Na bila shaka, daima kuna chaguo la kutembea.

Chagua pakukaa: Kama ilivyo kwa mapumziko ya bahari na mijini, chaguo ni nyingi. Lakini nchi ambazo ni ngome za ufahamu wa mazingira zinapaswa kuwa juu ya orodha yako. Norway, ambayo mara nyingi huchukuliwa kuwa moja ya nchi endelevu zaidi ulimwenguni, inaweza kuwa chaguo nzuri. Angalia hasa, Gala Fjellgrend katika Mkoa wa Skii wa Peer Gynt, unaojivunia vibanda vya mbao vya zamani na vilevile ufikiaji wa miteremko ya kuvutia ya hadi kilometa 30.

Popote unapochagua kwenda na chochote unachochagua kufanya, weka akili yako kwenye kufanya maamuzi sawa  kuitunza sayari yetu, na utakuwa sawa. Na kuwa na furaha!

habari mpya
spot_img
Related news