Saturday, June 3, 2023

Maadili ya QNET

Mazoea ya uuzaji wa kitaalam ni lazima katika biashara ya QNET.

Gundua jinsi tunavyohakikisha kuwa Wawakilishi wetu Huru wanazingatia sheria na kanuni za QNET.

  • Je! Mnadhibiti aje shughuli za wawakilishi wenu wa mauzo? Wote wako huru?

Kwa mara nyingine, ni muhimu kukumbuka kuwa Wawakilishi Huru (IRs) sio wafanyikazi wa kampuni hii, kwa hivyo hawafai kuitwa ‘wawakilishi wa mauzo’. Wao ni wawakilishi wa kujitegemea wanaoendeleza biashara zao wenyewe. Kama kampuni, QNET daima inahakikisha sheria na kanuni za maeneo zinafuatwa.

Mteja anapoamua kuwa Mwakilishi Huru, lazima asaini na akubali hati kamili ya Sera na Taratibu ambayo hutoa miongozo ya kufanya biashara kwa maadili. Kampuni hutoa bidhaa za kuboresha uuzaji kama gazeti, majarida, vipeperushi, wasifu wa bidhaa na video zinazosaidia Mwakilishi Huru kutangaza bidhaa za QNET.

SISI hufanya mafunzo ya kila mara katika nchi tofauti kuelimisha Wawakilishi Huru kuhusu mpango wa fidia wa QNET, mtindo wa biashara, bidhaa na muhimu zaidi, umuhimu wa uuzaji wa maadili na utaalam.

Pia kuna miongozo ya kimaadili na ya kitaalam, ambayo Wawakilishi Huru wote wanapaswa kuzingatia bila ubaguzi. Ikiwa masuala ya nidhamu au mengine yataibuka tutazishugulikia kwa ukali. Hatua za nidhamu zinaweza kuwa kama kueleza mlalamishi sababu mashtaka yaliyotolewa, na kusababisha kusimamishwa na/au kukomeshwa kazi.

Pia tuko na Idara ya Utekelezaji wa Mtandao (“NCD”) ambayo imepewa jukumu la kufuatilia mwenendo wa Wawakilishi Huru mtandaoni na kuhakikisha kuwa wanafanya biashara yao kwa weledi na maadili. NCD huchunguza malalamishi au madai yote dhidi ya Wawakilishi Huru wetu, na hatua inayofaa inachukuliwa kulingana na matokeo ya uchunguzi.

 

  • Je! QNET inafanya nini kuzuia uuzaji bovu na upotoshaji?

QNET iko na kanuni kali za kulainisha tabia za Wawakilishi Huru. Pia tuko na programu ya mafunzo yenye mada, QNETPro ambayo inazingatia kuwafundisha Wawakilishi Huru misingi ya biashara ya QNET, Mambo unaweza kufanya na usiyoweza kufanya, kujenga biashara endelevu kupitia mazoea ya kimaadili na kuwa kiongozi mtaalamu wa biashara.

Katika QNET, tunafuata sera kali ya kutovumilia uwakilishi wowote mbaya au mazoea yasiyo ya kimaadili kutoka kwa Wawakilishi Huru (IR) wanaotangaza biashara zao. Malalamiko ya kweli hushughulikiwa kwa uthabiti. Kwa kweli, kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita, kampuni yetu imesimamisha zaidi ya Wawakilishi Huru 750 ambao walikiuka sera na taratibu zetu. Tuko na mfumo wa urekebishaji unaoshughulikia malalamiko yoyote ya kila Mwkilishi Huru/mteja pamoja na upotoshaji wa Mwakilishi Huru. Kuna idara ya utekelezaji inayochunguza jinsi Wawakilishi Huru wanatumia mtandao.

Lakini, tunaweza tu kuchukua hatua ikiwa malalamiko yamewasilishwa kwa kampuni. Tuko na sera wazi ya kurudishiwa pesa kabla ya siku 30. Ikiwa mtu amekulaghai na ukanunua bidhaa na kusajiliwa kama msambazaji bila kutambua unayojihusisha nayo, unaweza kutamatisha mkataba wao na sisi kabla siku 30 baada ya ununuzi hazijaisha, na kutupea maelezo ya mtu aliyekupotosha. Tutakurejeshea pesa yako na tutachukua hatua zinazofaa dhidi ya mtu aliyekupotosha.

 

  • Je! Wawakilishi wetu wa mauzo wanalazimika kulipa ushuru?

Wawakilishi wetu Huru wote wanaelekezwa kwa kutumia sheria na kanuni za nchi wanamoishi na kufanya kazi. Ni wajibu wao kulipa ushuru, kama inavyotakiwa na sheria za nchi yao. Hii imewasilishwa katika Sera na Taratibu zetu.

 

  • Ni nani anayehusika na kutatua maswala ya mteja wakati kuna shida, QNET au Mwakilishi Huru wako?

Ikiwa mteja yeyote ako na malalamishi kuhusu bidhaa au huduma, QNET itachukua jukumu kamili kwa jambo hilo. Tuna kituo cha mawasiliano cha wateja wa lugha nyingi ambacho kinashughulikia malalamiko ya wateja kupitia simu na barua pepe. Maelezo ya huduma ya msaada kwa wateja wetu, inayojulikana kama Kikundi cha Usaidizi Ulimwenguni (GSG), zinapatikana kwenye tovuti yetu. Kwa sasa tunahudumia wateja wetu kwa lugha 15.

 

  • Je! Wawakilishi huru wako huru kuamua bei ya bidhaa?

Wawakilishi Huru wetu ‘hawauzi’ bidhaa na huduma kwa njia ya jadi. Ni lazima tu waelekeze wateja ili wanununue bidhaa na huduma kisha watalipwa ikiwa huyo mteja atanunua bidhaa au huduma kulingana na mpango wetu wa fidia. Bei ya bidhaa zetu haziwezi kubadilishwa. Wawakilishi huru wetu hawana uwezo wa kuamua bei kwa njia yoyote. Mteja mgeni hufanya ununuzi moja kwa moja kutoka kwa kampuni.

habari mpya
Related news