Saturday, June 3, 2023

Jinsi Ya Kuonyesha Wema Katika Biashara Yako


Je, ungependa kuonyesha wema katika biashara yako lakini hujui pa kuanzia? Umefika mahali pazuri. Siku hii ya Matendo ya wema, fanya bidii kua sehemu ya kujaza ulimwengu na wema kidogo kwa kuhusisha ubinadamu katika kila kitu unachofanya. Ikiwa miaka miwili iliyopita imetufundisha chochote, ni kwamba tunaweza kushinda chochote tunapokutana pamoja kama jumuiya. Weka ubinadamu na watu mbele kabla ya faida.

Kufanya Wema Katika Biashara Yako Kuwa kitu cha Kawaida

Njia bora ya kufanya ulimwengu kuwa mahali pazuri ni kuwa mkarimu mwenyewe. Kwa kufanya wema kuwa kitu cha kawaida katika jinsi unavyofanya biashara yako, unaweza kuhamasisha wengine kutaka kuwa kama wewe. Ni vyema kuchukua hatua nyuma na kutenda wema na kuifanya kuwa sehemu ya maadili ya kazi yako.

Jali Wengine

Tambua mawazo, hisia, matendo na maneno ya watu wengine. Sikiliza kwa bidii na uone watu wengine wanasema nini. Jaribu kuelewa maoni yao na utengeneze nafasi salama ambapo wanaweza kushiriki mawazo yao na wewe. Dumisha mahusiano kwa kuwacheki mara kwa mara ili kujua wanaendeleaje. Na muhimu zaidi, kua sehemu ya RYTHM na ujitoe kwa jumuiya unakoishi.

Wategemee timu yako

Leaning On Your Team QNET Success Tips.png?compress=true&quality=80&w=1024&dpr=1 Ufahamu Wa QNET

Kubali kua una hofu ya kuwa “mzigo” na jiruhusu kuegemea/kutegemea Familia yako ya QNET na marafiki. Omba ushauri kutoka kwa timu yako na viongozi wako. Usiogope kuomba msaada unapohitaji. Uongozi ni kuhusu muunganisho na ushirikiano, na timu yako itafurahi kukusaidia jinsi unavyoisaidia. Ili kuongeza ukarimu katika biashara yako, ongea na kuwa wazi kuhusu jinsi unavyohisi.

Sherehekea mafanikio madogo madogo

Maendeleo ni maendeleo, haijalishi ni madogo kiasi gani. Je, unakumbuka hundi yako ya kwanza na jinsi ilionekana kuwa jambo kubwa kwako wakati huo? Kua na hisia hizo hizo na ushangilie kila ushindi mdogo Pamoja na timu yako. Kwa kweli, kuweka kumbukumbu zako karibu na kushindwa ni wazo nzuri kwa sababu daima ni mawe ya hatua kwa mambo makubwa zaidi. Tenga muda wa matukio na uongeze wema katika biashara yako.

Anza kujipenda Zaidi

Kindness In Your Business - QNET Self-Love Calendar 2022

Fuata Kalenda ya Kujipenda ya QNET ili kufanya mazoezi ya kujipenda mwaka huu. Fanya kuwa mazoea ya kuwa mkarimu kwako mwenyewe na kuchukua wakati kwa ajili ya afya yako ya akili na kimwili. Sikiliza kitabu unachopenda, tazama kipindi unachopenda, fanya mambo unayopenda na uongeze furaha maishani mwako.

habari mpya
Related news