Wednesday, May 31, 2023

Mafunzo tano ya uongozi kwa wauzaji wa moja kwa moja kupitia Soka

Tunaweza kujifunza mbinu mbalimbali za uongozi kutoka kwa mpira wa miguu ambazo  tunaweza kutumia katika safari yetu ya uuzaji wa moja kwa moja. Moja ya sababu QNET ikawa mshirika rasmi wa kuuza moja kwa moja wa timu ya Manchester City, ni muunganiko wa upendo na heshima wa mchezo huo na maadili yake.

Masomo tano muhimu ambayo unaweza kujifunza kupitia soka:

  • Weka Malengo yako

Kujenga biashara endelevu inahitaji fikira za mikakati ya muda mrefu. Hiyo inamaanisha kuweka malengo na kuchukua hatua kwa vitendo -Kama ilivyo kwenye mpira wa miguu. Kuanzia malengo ya kujaribu kufunga magoli wakati wa kila mechi, hadi malengo ya kushinda Ligi au hata Kombe la Dunia, unaweka malengo na kuyafanyia kazi kwa bidii kama timu.

  • Kiongozi Mzuri ni sawa na Timu yake

Na kinyume – utendaji wako na ule wa washiriki wa timu yako unategemeana. Mtazamo au uwajibikaji wa kila mshiriki wa timu hutimiza lengo la pamoja. Ikiwa haujali kama kiongozi, basi usishangae ikiwa timu yako haikuchukui kwa uzito. Ikiwa unajali timu yako, utashangaa ni jinsi timu yako inakujali.

 

  • Huwezi Kushinda Peke yako

Kwenye michezo na maishani, huwezi kushinda peke yako. Hata katika michezo ya kibinafsi, bado unaye mkufunzi na watu kwenye kona yako. Kipa hawezi kuzuia ushambulizi wote peke yake – anahitaji mabeki. Uuzaji wa moja kwa moja ni biashara ya watu – tunaunda mtandao wa kuuza bidhaa tunazoamini, maana yake ni biashara ya kushirikiana. Haiwezi kuwa kiongozi bila kuwa na timu ya kuongoza!

  • Uongozi wa kuigwa

Hauwezi kuzungumza bila kufanya matendo kama vile huwezi kuzungumzia mchezo mzuri bila kucheza. Katika QNET, moja ya maadili yetu ya msingi ni uadilifu, na hiyo inamaanisha kutimiza jukumu lako kwa uwezo wako wote. Kama nahodha, ni kazi yako kuonyesha ubora ndani yako na kuleta ubora katika timu yako.

  • Kujitolea

Kufanya kazi katika timu na kufanya kazi na timu hukufundisha mengi, lakini pia la muhimu zaidi ya yote ni jinsi ya kumtanguliza mtu mwingine zaidi yako wewe mwenyewe. Kuna washiriki 11 katika timu kwa kusudi – ikiwa mshambuliaji atakimbia uwanja mzima akiufukuza mpira, angechoka na kuwakabili wapinzani kumi peke yake. Fikiria kile timu yako inahitaji na lengo lako la pamoja kabla ya malengo yako binafsi. Ikiwa kila mtu anafikiria hivi, basi kila mtu aatajali  mwenzie… na ndivyo unavyoshinda.

Unafikiria ni masomo gani ya maana ya maisha ambayo unaweza kujifunza kutoka kwa soka? Hebu tuambie katika maoni hapa chini. Na usisahau kusambaza hili na timu yako!

habari mpya
Related news