Saturday, March 25, 2023

QNET na Microsoft: Waungana Katika Kuleta Mabadiliko Ya Kidijitali

Kwa miaka mingi, QNET na Microsoft zimeendesha mabadiliko makubwa ya kidijitali kwenye miundombinu ya IT ya QNET kwa wasambazaji na wateja kupata matumizi bora na salama mtandaoni. Afisa wetu Mkuu wa Habari Ivan Woo aliongoza mageuzi hayo, na kuhakikisha kwamba usalama wako wa mtandaoni unalindwa, na data yako inalindwa unapofanya biashara kama kawaida.

Je, Ushirikiano huu wa QNET na Microsoft Umewezesha kuimarisha Kazi Gani?

Sehemu ya kuimarisha Miundombinu ya IT ya QNET ilijumuisha kurahisisha masuluhisho ya matatizo ya kawaida. QNET na Microsoft walirekebisha mfumo mzima wa usalama ili usikabiliane na matatizo mengi ambayo tovuti nyingi za biashara ya mtandaoni na programu hukabiliana nazo. Hapa kuna faida kuu ambazo unaweza kuwa labda umegundua.

Uimara wa Mtandao

Mojawapo ya mambo mengi tuliyofanya wakati wa mageuzi haya ya miundombinu ni kwamba tulihakikisha kuwa haukabiliwi na wakati wowote unaoathiri miamala ya biashara yako au matumizi yako ya mtandaoni ukiwa kwenye tovuti ya QNET, QNET Virtual Office, eStore, na blogu hii. Tangu masahihisho, tuna mtiriko na zana bora, ili kufanya utumiaji wako wa mtandaoni kua thabiti na bora zaidi.

Kuongezeka kwa Usalama Mtandaoni

Shukrani kwa QNET na Microsoft kwa urekebishaji wa miundombinu, timu ya usalama ya IT ya QNET inaweza kutathmini kwa vitendo na kuepusha matatizo ya mtandaoni. Wanaweza kudhibiti vitisho vinavyowezekana hata kabla ya wewe kutambua na kuripoti. Timu yetu sasa inajiamini sana katika kuwapa wasambazaji wetu nafasi bora na salama zaidi ya kutumia mfumo wa kidijitali bila uwoga, kufanya ununuzi, na mengine mengi.

Je! ungependa kujua zaidi? Sasa unaweza kusoma yote kuhusu safari hii ya QNET na Microsoft na kujifunza zaidi kuhusu Miundombinu yetu ya IT ya QNET na uboreshaji wake kwenye tovuti ya Microsoft. Usisahau kushiriki na marafiki zako na familia ya QNET!

habari mpya
Related news