Wednesday, May 31, 2023

Sayansi ya kuipa Ngozi yako muonekano ang’avu

Ubongo, moyo, mapafu, ini, na figo zote zinatambuliwa kuwa viungo muhimu. Lakini ngozi yetu – chombo kikubwa zaidi cha mwili – ni muhimu pia kwenye afya ya binadamu.

Kwa mfano, ingawa wengi wetu tunafahamu kuwa ngozi hutumika kama ganda la nje tu, ambalo halitambuliki kwamba pia hufanya kazi ya kuzuia dhidi ya vitisho vingi.

Kimsingi, wanadamu hukutana mara kwa mara na aina mbalimbali za ‘allergener’ na ‘pathogens’. Lakini, mara nyingi tunalindwa dhidi ya vitu vibaya kutokana na ngozi yetu – au haswa, seli maalum za ‘Langerhans’ zilizo ndani yake.

Ingawa, ngozi yetu kama viungo vingine, hupitia changamoto nyingi kila siku.

Kwa hivyo, ili kuhakikisha kuwa inafanya kazi kwa ufanisi, tunahitaji kuitunza vyema. Na moja wapo ya njia bora zaidi za kufanya hivyo, wataalam wanasema, ni kufahamu zaidi majukumu mbalimbali ya ngozi.

Hapa kuna baadhi yao:

Kuweka sawa joto la mwili

Kati ya kazi kuu moja wapo ya ngozi ni kutunza joto la mwili wetu. Hii inafanyika kwa njia mbalimbali zilizojengwa ndani ya miili yetu, ikiwa ni pamoja na kutoa jasho wakati wa joto.

Binadamu wana hadi tezi milioni 5 za jasho kwenye ngozi yetu, na mwili unapopatwa na joto, tezi hizi hutoa mchanganyiko wa maji, chumvi, na vitu vingine ili kutupooza/kuupoza mwili.

Ingawa jasho ni bora kwa kudhibiti Joto la mwili , uchafu uliojificha unaweza kusababisha ngozi yako kuharibika kama hauta ishughulikia ipasavyo.

Kwa hivyo, ni muhimu kua na utaratibu wa utunzaji wa ngozi yako kila siku ambao unajumuisha kuoga mara kwa mara na kunawa uso kwa kutumia vifaa maalum kama vile Physio Radiance’s Gentle Foaming Cleanser au DEFY Dirt Fighter ambayo sio tu ya kuondoa uchafu, lakini pia ni laini kwenye ngozi.

Zuia kupoteza unyevu nyevu wa Ngozi

Ukiachana na jasho, mwili hutoa sebum, mafuta yanayo linda ngozi na nywele kutopoteza maji na unyevu nyevu

Maji ni muhimu kwaajili ya viungo na tishu kufanya kazi vizuri, lakini tunapoteza maji mengi kila siku kutokana na sababu mbalimbali. ‘Sebum’ ni njia moja ambayo unatunza mwili/Ngozi kupoteza unyevu nyevu

Kuna tatizo moja lakini, hata hivyo, ni kwamba uzalishaji wa sebum hutofautiana baina ya watu. Kwa hivyo, tunahitaji kusaidia utengenezaji wa asili mwilini.

Njia chache za kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa tunakunywa maji ya kutosha, kula vyakula vyenye afya na pia kulainisha ngozi yetu kwa mafuta mazuri.

Physio Radiance’s Restoring Day Cream na Regenerating Night Cream, zinalenga kulisha na kuimarisha ngozi, kwa mfano, huleta suluhisho la muda mrefu.

Ulinzi dhidi ya mionzi ya UV 

Ngozi ya binadamu hubadilika rangi na kua yenye uweusi inapo chomwa na jua kwa muda mrefu. Na kwasababu hiyo, sayansi inatuambia, ‘melanin, rangi asilia inayolinda mwili dhidi ya miale hatari ya UV (Jua) ambayo inaweza kusababisha matatizo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na saratani ya ngozi.

Kweli, haimaanishi moja kwa moja kwamba kuchomwa kwa muda mrefu na jua husababisha saratani. Lakini, kilicho wazi ni kwamba tunapozeeka, ngozi yetu hupitia mabadiliko ambayo hudhoofisha ulinzi wetu. Kwa hivyo, suluhu ni kuhakikisha kuwa unalindwa kila wakati unapotoka kwenye jua.

Hakikisha umechagua kinga ya jua yenye ulinzi mpana kwa ajili ya hii, ambayo ni angalau SPF 40. Zaidi ya hilo, paka Physio Radiance’s Firming & Lifting Double Serum asubuhi na usiku ili kusaidia ngozi yako kurekebisha rangi ya Ngozi yako ambayo inakusababishwa wakati wa jua kali.

Husaidia kuzalisha vitamini D

Tukizungumzia mwanga wa jua, ngozi yetu ina jukumu muhimu katika kutoa Vitamini D, kitu ambacho ni muhimu kwa utendaji mzuri wa viungo na mfumo wa kinga.

Kwa kifupi, seli muhimu pokezi huishi kwenye ngozi zetu. Na mwanga wa jua vikiwapiga, husaidia miili yetu kutoa na kutengeneza Vitamini D.

Kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukaa ndani ya nyumba au sababu zingine zinazohusiana na aina za kipekee za ngozi – wengi wetu tunakabiliwa na upungufu wa Vitamini D bila kujua.

Kwa bahati nzuri, hili swala linaweza kutatuliwa. Unachohitaji kufanya ni kuongeza vyakula vyenye Vitamin D kwenye mlo wako, meza vidonge vya vitamini au kama iliyshauriwa na dakitari wako au hata pia kutumia krimu/mafuta sahihi.

Mfano, krimu ya Siku ya Physio Radiance’s Restoring Day Cream, imetengenezwa kwa mafuta matamu ya mlozi, kiungo asilia ambacho kina virutubishi vingi muhimu, ikiwa ni pamoja na Vitamini D.

Juu ya yote ni kwamba ngozi yetu inatufanyia mengi. Lakini kwa kweli tunahitaji kutunza vizuri ngozi zetu ili tuweze kuisaidia kutusaidia.

habari mpya
Related news