Wednesday, May 31, 2023

Vidokezo sita Muhimu Kuimarisha Uwasilishaji wako wa Biashara

Unataka uwasilishaji wako wa biashara kuinuka kutoka wastani hadi bora? Hivi ni vidokezo sita muhimu ambavyo tumeweka kukusaidia. Ikiwa unapata wasiwasi kabla ya mawasilisho yako au unahisi unaweza kufanya vizuri, vidokezo hivi 6 vitakusaidia kujifunza jinsi ya kuhakisha uwasilishaji wako wa biashara unaofuata unakua wa viwango vya juu na pia kukupa zana za kujenga msingi thabiti popote unapowasilisha, na chochote kinachozungumziwa.

  • Chagua Ukumbi unaofaa 

Kuchagua ukumbi unaofaa sio rahisi kama kuchagua ukumbi uliyo ndani ya bajeti yako halafu kutokua na wasiwasi wa kingine chochote. Unahitaji kuzingatia ukumbi unaoweza kuchukua shauku yatimu yako ya QNET. Hii haimaanishi tu kuwa ukubwa kwa kipimo lakini pia kuwa katika maeneo ambayo hayato kerwa na shangwe zetu. Ukumbi unapaswa pia kuwekwa vifaa ambavyo vitasaidia uwasilishaji wa biashara yako kitaalam –  vipaza sauti na teknolojia ya uwasilishaji. Lakini zaidi ya hayo, ukumbi uwe na mwanga wa kutosha, na usambazaji wa hewa nzuri na mtandao mzuri.

Wakati wa uwasilishaji unapofika, fika mahali pa ukumbi kabla ya wakati ili kuangalia kwamba kila kitu kinafanya kazi, na pia kuwakaribisha wageni wako. Na kamwe usiondoke kwenye chumba wakati wa uwasilishaji au wageni wako wanaweza kukufuata. Pia huleta usumbufu  sana kwa wageni na wasemaji.

  • Kuwatambulisha na kukaribisha walio katika ngazi za juu na Washauri wako

Walio katika ngazi za juu au hata washauri wako, hao ni mataalam katika uuzaji wa mtandao, na haswa katika utafutaji. Kuwashirikisha ni njia nzuri ya kupata maoni juu ya nini unaweza kufanya vizuri zaidi na kile unapaswa kufanya zaidi. Jambo muhimu zaidi, unaweza kutumia mwongozo wao kwa njia ambayo watu wengi hawawezi. Kuwa nao hapo na kujua kwamba wakati mmoja walipitia jambo lile lile ulilofanya sio tu chanzo kizuri cha faraja lakini pia fursa ya kipekee ya kujifunza.

  • Kuwa Tayari, usiwe wa Kubahatisha 

Labda umesikia uwasilishaji wa QNET mara nyingi na unaweza kuwa umefanya mara kadhaa wewe mwenyewe. Lakini bila kujali una ufasaha gani katika Mpango wa Fidia wa QNET, kuwa na muhtasari wa uwasilishaji na kuufuata. Zingatia muda na kumbuka kufuata msimamo wa QNETPRO na tumia uwasilishaji rasmi wa QNET na vifaa vya mafunzo ili kuepuka upotoshaji wa bidhaa na fursa ya biashara.

Ukishajua utakachosema, anza mazoezi. Wasilisha mbele ya familia yako, marafiki zako, au hata mbele ya kioo. Unapozungumza zaidi, unaua mzoefu zaidi. Hii ni njia nzuri kwao kukupa maoni na kurekebisha mkao wako au hata yaliyomo.

  • Wajue Wasikilizaji Wako

Hakuna kitu ambacho watazamaji wanapenda zaidi ya msemaji ambaye anatambua mada anayozungumzia. Jifunze kadiri uwezavyo juu ya hadhira yako na usisitize uwasilishaji wako kuwaelekea. Ingawa ni kazi nyingi zaidi kuliko kuingia tu na kuzungumza juu ya QNET, ni bora kujua ni nini kinachowahimiza wasikilizaji wako, ni kiasi gani wanajua juu ya uuzaji wa moja kwa moja, au hata sababu yao ya kuhudhuria uwasilishaji wako.

Tambua vitu gani wasikilizaji wako wantaka kupata kutoka kwenye uwasilishaji wako na kisha ujenge hoja kulingana na mahitaji yao. Kumbuka kuwa uwasilishaji wako unahusu wasikilizaji wako na lengo lako ni kuwafanya wajifunze kitu, na kukuamini.

  • Mahudhurio yanapaswa kuwa ya hiari

Chochote unachofanya, USILAZIMISHE watu kuhudhuria uwasilishaji wako endapo atakataa kuhudhuria. Na kamwe usilazimishe mtu yeyote kukaa katika mawasilisho yako ya biashara kinyume na mapenzi yao. Watu wana uwezekano mkubwa wa kuwa na nia wazi juu ya fursa hiyo ikiwa watatambua kuwa wana chaguo na, mwishowe, uamuzi ni wao wenyewe.

  • Jipambe kwa Halfla hiyo

Hapana, hatuvai suti kamili. Lakini kumbuka kuwa hii ni mada ya biashara, na kwa hivyo unahitaji kuvaa ili kuvutia. Muonekano wa kwanza ni muhimu sana, na kwa hivyo, vaa vilivyo. Usivae suruali yako iliyofifia / iliyokatwa au fulana iliyo na picha za kuchekesha. Vaa kwa njia ambayo utachukuliwa kwa uzito badala ya kuonekana kama mhitimu mpya. Unapokuwa na shaka, vaa jean yenye rangi dhabiti na fulana yako uipendayo ya QNET

Fanikisha uwasilishaji wako wa biashara unaofuata kwa kutumia vitalu sita vya ujenzi ili kuvutia wasikilizaji wako, na uwape mawazo yako yaliyojaa maarifa. Baada ya yote, utangulizi bora kwa jamii ya QNET unaweza kukusaidia sana, wawakilishi wetu, kuongeza nafasi zako za kufanikiwa kama wajenzi wa biashara.

habari mpya
Related news