Saturday, June 3, 2023

Vidokezo vya kuwa na hali nzuri kazini

Tunajua kuendesha biashara ni kazi ngumu. Lakini utafiti unaonesha kuwa kwa ujumla, wajasiriamali ni watu wenye furaha. Na kwa nini wasiwe?

Sio kila mtu anaweza kujiajiri. Kwa hivyo kuweza kujinasua kutoka kwenye pingu za kuajiriwa kwenda na kufuata ndoto zako na kutengeneza biashara kwa kweli huleta sababu za kutabasamu.

Hata hivyo si mara zote ni rahisi.

Wajasiriamali wengine husema kuwa na biashara inahusisha kujitolea na kujitoa sana kiasi kwamba mara nyingi mtu anaweza kusahau kutazama upande mzuri wa maisha.

Ikiwa huyu ni wewe, pengine ni wakati wa kubadilisha mambo na kuwa na mtazamo mpya kazini.

Hapa kuna vidokezo vitano vya kuongeza hisia zako kazini.

Anza siku yako vizuri

“Amka na uangaze” ni zaidi tu ya msemo. Ni mtazamo uaotengeneza siku yako. Jambo ni ,kuanza siku yako vizuri kunahitaji, kupumzika usiku vizuri.

Je ,mara nyingi huamka na uchovu zaidi? Wauzaji wengi wa moja kwa moja  na wamiliki wa biashara wana mambo mengi mno,na kwamba hawapati usingizi wa kutosha.

Lakini , kupumzika ni ufunguo wa kuamka vizuri na kuwa na furaha katika siku yako kazini. Kwa hivyo anza kuzingatia kupumzika vizuri.

Unataka kujipa mwanzao wa furaha zaidi? Usiangalie simu yako asubuhi!

Badala yake, jaribu kwa ukimya kuonesha shukurani kwa baraka zako na kisha, amka.

Ipange siku yako

Ili kuhakikisha ufanisi mkubwa, unapaswa kuanza siku yako kwa kuandaa na kupangilia kazi zako.

Wajasiriamali bora wanajua kuwa kila dakika ni muhimu. Na hakuna kitu cha kusisitiza zaidia kuliko kuhitimisha kazi.

Pia, ikuhakikisha kuondoa shida, jaribu kufanya kazi kwa mpangilio wa umuhimu.

Hili linaweza kuonekana kuwa la kuchosha, lakini inasaidia kukumbuka kuwa kukamilisha kazi kwenye orodha huongeza furaha ya mtu, hivyo kukuacha usiwe na uchovu na uchangamfu zaidi kwa siku nzima.

Chukua mapumziko

Kuzingatia kukamilisha kazi, hata hivyo haimaanishi kumaliza siku bila mapumziko yoyote.

Kwa ufanisi wa juu zaidi, inashauriwa kupumzika kati ya mikutano mingi na kuongea na wateja ambayo umeweka kwenye ratiba zako.

Hakika, wakati mwingine kupumzika kunaweza kuonekana haiwezekani kutokana na kazi zote zinazohitajika kukamilika katika siku.

Lakini sayansi iko wazi- kumpunzika  mara kwa mara kwaajili ya kupata chakula cha mchana, kwenda kufanya mazoezi au hata kufunga macho kidogo humfanya mtu kuwa mtulivu na, kwa hivyo, kuleta tija zaidi.

Kwa kweli, mafanikio hayaji bila kujitolea kamili. Lakini kujitoa pia kunamaanisha kujitolea kwa afya na furaha yako.

Rekebisha

Jambo lingine ambalo wakati mwingine hupuuzwa kuwa halina maana katika kuamua hisia zako ni mazingira ya kazi yako.

Je, ofisi yako ni angavu na yenye hewa? Je , imejazwa na mimea ya asili? Je , unakiti au meza sahihi?

Hakuna suluhu ngumu na za haraka kwa aina gani ya ofisi inahakikisha tija na raha. Lakini ikiwa umekuwa ukijihisi kutotiwa moyo ukiwa kwenye meza yako, unweza kuwa ni wakati wa kurekebisha mambo.

Punguza vitu. Weka mchoro/picha mpya. Paka rangi kama kijana uan njano(kutuliza kwa kijani, njano ya kuinua) weka mmea kwenye dawati lako.

Chochote unachochagua kufanya ili kuboresha mambo, hakikisha kuwa kunakufaa.

Lenga, shinda , sherekea

Ikiwa kunapanga siku nzima ya kazi ni muhimu, pia kuzingatia malengo yako ya siku na kile unachonuia kufikia.

Wajasiriamali, bila shaka, wana picha ya wapi wanataka kwenda na jinsi ya kufika huko. Lakini kama mmiliki yeyote wa biashara anaweza kuthibitihsa mafanikio sio mstari ulinyooka, na kuna vituo vingi na mwanzo mwingi.

Kwa hivyo usisahau kusherekea hatua ndogo katika siku yako ya kazi.

Labda umeweza kufunga dili na mtarajiwa ambaye hapo awali alisita kufanya kazi na wewe. Labda mtu wako wa chini ameweza kuchukua uongozi kwenye mradi na kuleta matokeo ya kuvutia.

Kila kitu kinafaa kutambuliwa na kusherekewa, zaidi sana ikiwa inakupa furaha huku ikikufanya uhisi matumaini na furaha.

 

 

habari mpya
Related news